Friday, May 4, 2012

KIVUMBI KUTIMKA KESHO UWANJA WA SEMINARI

Na Mkula Kennedy

Mashindano ya FAWASCO katika chuo cha MT. Agustino yaendelea kesho katika uwanja seminari katka hatua ya robo fainali ambako kutakuwa na mpambano mkali kati ya  Eduche II Vs Ada, ikifuatiwa na PR III Vs LLB III.

Mashindano hayo yanaanza tena baada ya mapumziko ya muda mrefu baada ya hatua makundi kumalizika.Mechi ya kwanza itakuwa kati ya mabingwa watetezi wa mashindano hayo Eduche II Vs Ada saa 2:00 mchana.Huku mchezo wa pili ukiwa ni kati ya PR III Vs LLB III mnamo maijra ya saa 4:00 jioni.

Akiongea na washabiki wa mchezo huo, aliyekuwa Naibu Waziri wa michezo chuoni hapo, George Nkini alisema mechi hizo zilikuwa zifanyike katika uwajna wa Raila Odinga lakini kwa kuwa siku hiyo kutakuwa na Faculty Day Uongozi ukaamua mechi hizo zifanyike katika uwanja wa Seminari.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, kocha mkuu wa timu ya PR III, Robert Muhando amesema wachezaji wake wako tayari kupambana kwa kuwa wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo wa kesho na hakuna mchezaji yeyote ambae ni majeruhi, "Vijana wangu wana hari ya kushinda,wanajiamini na wako tayari kupambana", alisema Muhando huku akiwahakikishia washabiki wake kushinda mchezo huo.

Mashindano hayo yataendelea siku ya jumapili katika uwanja wa Raila Odinga kwa michezo miwili tofauti kati ya Eduche III Vs PR II saa 2:00 mchana ikifuatiwa na Mass Comm Vs LLB II saa 4:00 jioni.



No comments:

Post a Comment