MWENTEKITI MCT ATEMBELEA RADIO SAUT
Na Mkula KennedyMwenyekiti wa baraza la habari (MCT) Jaji Thomas Mihayo pamoja na wanachama wa baraza hilo, jana walitembelea Radio SAUT fm iliyopo Malimbe katika chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT).
Ziara hiyo ilifanyika siku moja kabla ya siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambao kitaifa imefanyika leo jijini Mwanza.
Mwenyekiti Mihayo, akizungumzia uhuru wa vyombo vya habari alisema Serikali inayotoka kwenye mfumo wa chama kimoja inatabia ya kuogopa vyombo vya habari pamoja na mahakama kwani ndio kimbilio la wanyonge.
Katika mazungumzo yake Mwenyekiti Mihayo aliipongeza Radio SAUT kwa kuwasaidia wanyonge ambao hawawezi kupaza sauti zao na kusikika.
Pamoja na hayo mwenyekiti huyo alitoa wito kwa watangazaji wa Radio SAUT pamoja na wanafunzi wa mawasiliano ya umma kutetea taaluma ya waandishi wa habari pamoja na kutunza maadili ya taaluma hiyo.
Awali katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Radio SAUT, Dotto Bullende, wanafunzi na watangazaji wa radio hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali ikiwa ni njia ya kupata uzoefu na ujuzi zaidi katika fani hiyo.
No comments:
Post a Comment