Tuesday, April 3, 2012

NAFASI ZA KUJIUNGA NA REMEDIAL PROGRAMME.

TANGAZO

Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania kinawatangazia nafasi za kujiunga na Remedial Programme kwa
mwaka wa masomo 2012/2013.Kozi hii ni kwaajili ya wale wote ambao alama zao hazifiki kiwango cha 4.5
katika kidato cha sita, ilikuwawezesha kupata elimu ya ziada iwasaidie kuendana na wanafunzi wenzao walio pata alama zaidi ya 4.5 katika kidato cha sita.


Sifa za Muombaji:


1. Awe amemaliza kidato cha sita.


2. Awe na Principal Points kuanzia 2.5 hadi 4
kwenye masomo mawili ya kidato cha sita (mfano: EE, DE, CE, DD, EEE na masomo mengine kuwa na S).


3. Gharama ni Tshs. 390,000/= (Tuition Fee) kwa miezi 3, malazi (accommodation) ni Tshs. 70,000/=, chakula ni kujitegemea.


4. Wale wote wenye sifa hizo watakao chaguliwa na TCU kuja SAUT watatakiwa kufika chuoni miezi mitatu kabla ya tarehe ya kujiunga chuoni kwaajili ya kuanza masomo ya remedial.


5. Kozi hii itaanza tarehe 2/7/2012.


Fomu zinapatikana ofisi ya Admissions na kwenye tovuti http://www.saut.ac.tz. Baada ya kumaliza kujaza
fomu zirudishwe ofisi ya Admissions-SAUT. Wahitimu wataruhusiwa kujiunga na vyuo vyote vilivyo chini ya SAUT ambavyo vinatoa programmes husika.


Wote mnakaribishwa.


Admissions Officer
BY; MROPE, Hassani.

No comments:

Post a Comment